KINSHASA:WATU 163 WAMEKUFA MAJI CONGO
28 Novemba 2003Matangazo
Kivuko cha ziwa kilichofurika watu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kimepinduka na imaaminika kwamba watu wasiopunguwa 163 wamekufa maji. Wengine madarzeni hawajulikani walipo. Wavuvi katika Ziwa Mai-Ndombe waliwasaidia kuwaokowa zaidi ya watu 200 waliochupa kwenye mashua hiyo ya kivuko wakati ikipasuka pande mbili kutokana na dharuba kali hapo Jumanne. Madaktari wa Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka na wale wa chama cha Msalaba Mwekundu wanasaidia kutafuta watu na kuwaokowa. Treni moja pia imeanguka mtoni hapo Jumaatano kutokana na maporomoko ya ardhi karibu na Matadi.Watu 11 hawajulikani walipo.