KINSHASA. Vurugu zazuka nchini Kongo.
18 Mei 2005Matangazo
Takriban watu wawili wameuwawa kufuatia maandamano yaliyofanywa na mamia ya wafuasi wa upinzani kusini mwa jimbo lenye madini katika jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Waandamanaji hao waliweka vizuizi barabarani na kuwarushia mawe polisi huku wakizichoma moto ofisi mbili za vyama vya kisiasa katika mji wa Mbuji Mayi ulio kilomita 900 kusini mashariki mwa Kinshasa.
Mkuu wa mkoa bwana Dominique Kanku amevieleza vyombo vya habari kwa njia ya simu kuwa huenda watu wengine watano wamejeruhiwa katika maandamanao hayo ambayo baadae yalizimwa na wanajeshi wa serikali.