KINSHASA : 26 wapoteza maisha kwenye maandamano ya Congo
2 Julai 2005Takriban watu 26 wamuwawa hapo Alhamisi wakati polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilipovunja maandamano kwenye miji kadhaa.
Serikali ilisema watu 10 wamekufa wakati polisi ilipovunja maandamano hayo ya upinzani kwenye miji kadhaa.Chama kikuu cha upinzani UDPS awali kilitowa idadi hiyo hiyo ya vifo lakini hapo jana kiliongeza idadi hiyo zaidi ya maradufu.
Joseph Mukendi msaidizi mwandamizi wa kiongozi wa UPDS amesema watu sita wameuwawa katika mji mkuu wa Kinshasa na zaidi ya 20 wameuwawa kwenye majimbo mawili makuu ya kati huko Kasai.
Maandamano hayo yalifanyika kupinga kushindwa kuitisha uchaguzi kama ilivyokuwa imepangwa awali kwa kuzingatia mkataba uliotiwa saini na serikali na makundi ya waasi hapo mwaka 2003 ambao ulikomesha vita vya miaka mitano vilivyosababisha maafa makubwa.