Kimbunga Wipha kimetatiza safari za ndege Hong Kong
20 Julai 2025Matangazo
Viwanja vya ndege huko Hong Kong, Shenzhen, Zhuhai na Macao vilifuta na kuahirisha safari zote za ndege za siku pamoja na safari za treni za mwendo kasi.
Shirika la uangalizi la Hong Kong lilitoa tahadhari ya viwango vya juu vya kimbunga Wipha, likionya kwamba kimbunga hicho kikali kitapita kwa upepo mkali wa kasi ya kilomita 140 kwa saa.
Maelfu wahamishwa China kufuatia kimbunga Wutip
Serikali tayari imesema watu zaidi ya 200 wamekimbilia katika maeneo salama huku ikiripoti kuanguka kwa miti mingi. Maeneo ya burudani kama Dysneyland mjini Hong Kong pia yamefungwa.
Kimbunga Wipha, kilipitia ufilipino kwa upepo mkali na kupiga pia sehemu kadhaa za Taiwan hapo jana Jumamosi (19.07.2025).