Kimbunga chaua zaidi ya watu 20 kusini mwa Marekani
17 Mei 2025Matangazo
Zaidi ya watu 20 wamekufa baada ya dhoruba kali kuyakumba majimbo ya kusini mwa Marekani ya Missouri na Kentucky. Hayo yamesemwa leo na maafisa pamoja na vyombo vya habari katika maeneo hayo.
Gavana wa Kentucky Andy Beshear ameandika kwenye mtandao wa X kwamba watu 14 wamekufa kutokana na kimbunga kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Watu wengine saba wamekufa huko Missouri, kulingana na gazeti la Washington Post.
Kwa mujibu wa gavana huyo idadi hiyo ya vifo huenda ikaongezeka.
Maeneo mengine kama Wisconsin na Texas pia yameathirika na kimbunga hicho ambapo duru zinasema kimepelekea karibu watu laki moja kukosa huduma ya umeme katika maeneo hayo.