JangaAustralia
Kimbunga Alfred chalazimu maelfu kuhamishwa Australia
7 Machi 2025Matangazo
Kimbunga hicho kinachosafiri kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa tayari kimeleta balaa kwenye majimbo ya Queensland na New South Wales usiku wa kuamkia leo. Usambazaji wa umeme umetatizika, fukwe zimechimbuliwa kwa wingi wa maji na viwanja vya ndege vimefungwa.
Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa imesema Kimbunga Alfred kinachoambatana na mvua kubwa kitakuwa na kasi kubwa zaidi kitakapowasili mji wa kaskazini wa Brisbane ambao ndiyo wa tatu kwa wingi wa watu nchini Australia.
Waziri Mkuu wa Australia Antony Albanese amewataka raia wa nchi hiyo kuwa makini na kuepuka kufanya matembezi ya kitalii au kutaka kwenda kujionea hali inavyokuwa wakati wa kimbunga