Kim akosoa ushirikiano wa Marekani, Korea Kusini na Japan
10 Februari 2025Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekosoa ushirikiano wa kiusalama kati ya Marekani, Korea Kusini na Japan akisema ni kitisho kikubwa kwa nchi yake na kuapa kuimarisha zaidi mpango wake wa silaha za nyuklia.
Katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 77 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi wa Korea mwishoni mwa juma hili, Kim alisema ushirikiano huo wa kiusalama wa nchi tatu, ulianzishwa chini ya njama ya Marekani ya kuunda kambi ya kijeshi ya kikanda kama ile ya jumuiya ya NATO. Kim Jong Un akosoa ushirikiano wa kiusalama wa pande tatu
Ameongeza kusema ushirikiano huo unaibua ukosefu wa usawa wa kijeshi kwenye Rasi ya Korea na changamoto kubwa kwa usalama wa nchi yake.
Rais wa Marekani Donald Trump alidokeza juu ya kutaka kufanya mazungumzo na Kim huku akijivunia mkutano baina yao wakati wa muhula wake wa kwanza.