Kila upande wavutia kwake katika mazungumzo ya DRC
14 Julai 2025Miaka mitatu imetimia tangu waasi wa M23 walipoanza kuyakamata maeneo ya mkoa wa Kivu Kaskazini, na kuwaweka wakaazi wa maeneo hayo katika matatizo chungu nzima. Wakaazi hao ambao wanaelezea kuchoka na hali hii, wanatarajia kuwa mazungumzo baina ya serikali ya Kinshasa na waasi yatafikisha mwisho uhasama na kuleta utulivu, kama anavyoeleza hapa Nene Bintu Iragi, kiongozi wa mashirika ya kiraia jimboni Kivu Kusini.
"Watu hawaishi tena kama binadamu. Mauaji yanaendelea, na kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Hali ni ya kutisha. Tunaona wapiganaji wengi wa AFC-M23 wakipelekwa kwa wingi mstari wa mbele, lakini pia wanajeshi wa serikali, FARDC wanajizatiti. Haiwezekani watu kufanya mazungumzo huku majeshi yakiendelea kurundikwa," alisema Nene Bintu Iragi.
Kulingana na chanzo kilicho karibu na mazungumzo ya Doha, AFC-M23 wanataka serikali ya Kinshasa iondoe vikwazo vilivyowekwa dhidi yao, ifute mashitaka, hukumu na maamuzi mengine ya kisheria dhidi ya viongozi wa waasi hao, iwaachilia mara moja waliokamatwa kwa tuhuma za kushirikiana na AFC-M23, na ikomesha na pia iadhibu kauli za chuki, na kusaini makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mapigano.
Serikali ya Kongo yasema kuna matumaini ya kufikiwa makubaliano
Juhudi za idhaa hii za kutafuta maoni ya serikali hazikuzaa matunda. Hata hivyo, katika chama cha UDPS cha Rais Félix Tshisekedi, kimesema kuna matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano ya haraka ili kupunguza mateso ya watu wa mashariki, kama anavyoeleza hapa Christian Lumu Lukusa, afisa wa chama hicho.
"Kwa zaidi ya miongo mitatu, eneo la mashariki ya nchi limekuwa likikumbwa na mauaji, ubakaji, na kuwahamisha watu kwa nguvu. Jambo la muhimu zaidi ni dhamira ya kila upande kufanya kazi kwa ajili ya amani ya kudumu kwa sababu watu wetu wameteseka sana. Wakati umewadia wapate ahueni."
Makubaliano ya amani kati ya DRC na Rwanda yakabiliwa na mashaka
Kupata amani ndio rai kuu kwenye vinywa vya raia wa Kongo, hususan wale kutoka mikoa ya mashariki. Lakini baadhi ya wachambuzi bado hawaamini kuwa mazungumzo ya Doha yataleta suluhu ya kudumu. Fred Bauma, Mkurugenzi Mtendaji wa Ebuteli, Taasisi ya Utafiti ya Kongo kuhusu Siasa, Utawala na Vurugu, ana maoni haya.
"Pande zote mbili—hasa M23, lakini pia serikali ya Kongo kwa kiwango fulani—zina masharti ya msingi ambayo ni magumu sana kutekelezwa. Nafikiri yote pia yatategemea ushawishi wa wasuluhishi na wadau wengine walioko, wakiwemo Marekani. Je, kila kitu kitakachosainiwa kitaweza kuheshimiwa? Watu wengi wanatia shaka. Lakini kile ambacho watu wanataka mwishowe ni amani, na bado hatujafika hapo."
Mawaziri wa mambo ya ndani wa Kongo na Rwanda pia wanashiriki katika maz (SW): Kila upande unav... ungumzo ya Doha. Mazungumzo haya ni hatua muhimu kufuatia makubaliano ya amani yaliyosainiwa kati ya DRC na Rwanda tarehe 27 Juni mjini Washington, Marekani.