Kuna ripoti kwamba mchakato wa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kukabidhi nafasi hiyo kwa Rais Magufuli umekuwa ukisuwasuwa kutokana na madai kuwa mwenyekiti huyo hataki au anachelewsha kwa makusudi.
Jambo hilo linalelezwa kuzusha mgawanyiko ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika. Kufuatia taarifa hizo DW imezungumza na msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka na kwanza ameulizwa yaliyotokana na kikao cha Kamati Kuu cha Mei 3 mjini Dodoma.