Kiini cha uhariri katika magazeti ya leo ya hapa Ujerumani ni ziara iliofanywa ...
4 Desemba 2003punde na Kansela Gerhard Schroader wa Ujerumani katika Jamhuri ya Umma wa Uchina. Suala lingine ni mazungumzo baina ya viongozi wa vyama vya wafanya kazi na waajiri ambayo hayajafanikiwa.
Othman Miraji anayakagua magazeti hayo:
Kuhusu ziara ya tano alioifanya Kansela Schroader huko Uchina, gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG lilikuwa na haya ya kuandika:
+Hata ingekuwa kinu cha kutengeneza nishati ya kinyukliya cha Hanau hapa Ujerumani hakiwezi kutumika barabara kwa malengo ya kijeshi, hata hivyo, namna na njia alioitumia Kansela Schroader kuwajibu wale watu waliokuwa na wasiwasi juu ya Uchina kuuziwa kinu hicho kunasema mengi. Mengi zaidi yanasemwa juu ya namna anavoitetea fikra ya kuondosha vikwazo ilivowekewa Uchina kupata silaha kutoka nchi za Muungano wa Ulaya. Kwa kansela lilo muhimu ni kwamba biashara inasonga mbele. Kansela huko Uchina alilifanya suala la haki za binadamu kuwa halina umuhimu, sio chochote sio lolote, hapa nchini Ujerumani. Yeye hajafahamu kwamba kuheshimiwa haki za binadamu ni shuruti ya kuwekeza vitega uchumi vy amuda mrefu huko Uchina. Nchi ambayo haizingatii haki za uhuru wa raia, inabakia kuwa ni nchi isiokuwa tulivu.+
Kwa ukali zaidi liliandika gazeti la BERLINER TAGESSPIEGEL na kumlaumu Kansela Schroader. Lilisema hivi:
+Hata ikiwa Wachina wengi hivi leo wanaonja uhuru zaidi, lakini haki za mtu binafsi bado zinaendewa sana kinyume. Maelfu ya wanachama wa madhehebu ya Falun-Gong wamewekwa katika makambi ya kazi ngumu, wengi wao hawataweza katika uhai wao kumaliza hayo yanayoitwa mafunzo wanayopewa ndani ya kambi hizo. Ikiwa Gerhard Schroader nje ya nchi hii analifanya suala la haki za binadamu kuwa ni suala la pembeni, ikiwa kansela huyo anatoa sura kwamba anakubaliana na namna Uchina inavoitishia kivita Taiwan ilio nchi ya kidimokrasi, basi kansela huyo na siasa yake ya kuelekea Uchina anafanya asiaminike.+
Gazeti la MANNHEIMER MORGEN lilizusha suali vipi Chama cha Kijani kitakavoyajibu matamashi hayo ya Kansela. Lilikuwa na haya:
+Kwanza: Kansela alitoa wazo la Uchina kuondoshewa vikwazo vya silaha ilivowekewa, na baadae akatangaza yuko pia tayari kutaka kuiuzia Uchina kinu cha Hanau cha kutengenezea nishati ya kinyukliya. Alifanya hivyo kana kwamba jambo hilo linafahamika wazi na viongozi wa Chama cha Kijani, kinachoshiriki naye serekalini. Gerhard Schroader anafikiri viongozi wa Chama cha Kijani wamekuwa sio wenye kuleta mabishano, wakimya. Hivyo ndivyo mtu anavodhania. Huenda hajaziumiza hisia za viongozi wa chama hicho, kwa vile Kansela huyo amefaulu kuendeleza biashara ya Ujerumani katika Uchina, lakini amesababisha uharibifu katika serekali yake ya msetio.+
BERLINER TAGESZEITUNG liliandika namna hivi:
+Ishara zilizopatikana kutokana na ziara ya Kansela ya kutangaza biashara ya Ujerumani ni ya wazi. Nayo ni kwamba kwa mujibu wa Kansela watu wanaweza kulalamika juu ya mzozo wa bajeti ya serekali yake hapa nchini na upunguzaji wa huduma za kijamii, lakini katika biashara ya nje yu tayari kuondosha vikwazo vyote vya kusafirisha nje bidhaa za Kijerumani. Nyumbani hata watu wanaomzunguka wamepigwa na butwaa, kutoka Tume ya Muungano wa Ulaya ya mjini Brussels hadi washirika wake katika serekali yake, yaani Chama cha Kijani. Na wale waliokuwa ndani ya chama chake wamenyamaa kimya. Lakini kutoka kesho, lazima Schroader ajaribu kuyasawazisha mambo, na hapo tena ataachana na matamshi yake ya kujititimua aliyoyatoa Uchina.
Kuhusu mazungumzo yalioshindwa baina ya viongozi wa vyama vya wafanya kazi na wale wa waajiri wa hapa Ujerumani, gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU liliandika hivi: + Waajiri walifikiri sana kwamba kutapatikana suluhu kwa vile waliungwa mkono na vyama vya upinzani vya CDU/CSU na FDP katika mapendekezo yao kwamba kuweko sheria ya kuruhusu kuweko mashauriano huru baina ya wafanya kazi wa viwanda fulani na waajiri wao. Kutokana na hali iliokuweko, jaribio hilo la kupata suluhusu lilikuwa wazi lishindwe. Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanya kazi la Ujerumani, Michael Sommer, alichukuwa dhamana kubwa pale alipoanza kushiriki katika mashauriano hayo. Kushindwa mazungunzo hayo ni hasara kwa kiongozi huyo.+