Kifaru cha Kimarekani chashambuliwa Iraq:
17 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD:
Nchini Iraq wameuawa wanajeshi watatu wa
Kimarekani na walinzi wa usalama wawili wa
Kiiraq kifaru cha wanajeshi wa Kimarekani
kiliposhambuliwa Kaskazini mwa mji mkuu
Baghdad. Wanajeshi wawili wengine wa
Kimarekani walijeruhiwa. Kifaru hicho
kilichokuwa kikiwachukua walinzi hao wa
Kiiraq waliokuwa wakifuatana na wanajeshi wa
Kimarekani, kilipita katika njia iliyotegewa
mripuko. Washutumiwa watatu wametiwa nguvuni.
Kabla ya hapo waliuawa Wairaq wawili
kiliposhambuliwa kituo cha ulinzi huko Iraq
ya Magharibi. Washambuliaji sita wameweza
kukamatwa.