Kifaru cha Kimarekani chashambuliwa Iraq:
18 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq wameuawa wanajeshi watatu wa Kimarekani na walinzi wa usalama wawili wa Kiiraq kifaru cha wanajeshi wa Kimarekani kiliposhambuliwa karibu ya Tadji, huko Kaskazini mwa mji mkuu Baghdad. Wanajeshi wawili wengine wa Kimarekani walijeruhiwa. Wanajeshi wote waliouawa walikuwa ndani ya kifaru hicho kilichopita katika njia iliyotegewa mripuko. Hivi sasa kimefikisha 500 kiwango cha Wajeshi wa Kimarekani waliouawa Iraq tangu vimalizike rasmi vita. - Pia katika ule mvutano wake kuhusu swali la kuikabidhi madaraka serikali ya Kiiraq, Marekani inazidi kutafuta msaada wa UM. Jumatatu ya kesho, Mtawala wa Kimarekani wa Mambo ya Kiraiya wa Iraq, Paul Bremer atafuatana na ujumbe wa Serikali ya Mpito ya Iraq kwenda kuzungumza na Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan mjini New York.