Hivi karibuni yalifanyika maonesho maalum ya wajasiriamali wa teknolojia wa Kiislamu jijini London nchini Uingereza. Moja ya vitu vilivyowavutia washiriki wengi katika maonesho hayo ni kifaa kinachosaidia kutambua Makka ilipo na mswala wa kidijitali maalum kwa kufanyia sala.