Kiev yakataa wazo la Putin, Zelensky kwenda Moscow
4 Septemba 2025Matangazo
Putin amesema kuwa alikuwa amejadili suala hilo na Rais wa Marekani, Donald Trump. Akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu afanye mkutano wake wa kilele na Trump wa Alaska, akiwa nchini China, Putin alisema "Donald aliniuliza kama inawezekana kuandaa mkutano wa aina hiyo. Nikamjibu: Ndiyo, hilo linawezekana.Zelensky anaweza kuja Moscow ikiwa yuko tayari. Kupitia ukurasa wake wa X, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, amesema takriban nchi saba zimejitolea kuwa wenyeji wa mkutano kati ya Putin na Zelensky. Na yuko tayari kusafiri mara moja kwenda katika mojawapo ya nchi hizo kwa ajili ya mkutano.