KIEV: Ukraine imepanga kuondoa majeshi yake nchini Iraq
2 Machi 2005Matangazo
Ukraine imepanga hadi kufikia katikati ya mwezi wa Oktoba, kuwa imeondosha majeshi yake nchini Iraq. Kwenye awamu ya kwanza, wanajeshi 150 wataondoka nchini humo, hapo tarehe 15-Machi, alisema rais wa Ukraine, VICTOR JUSCHT-CHENKO baada ya kikao cha baraza la usalama na ulinzi. Awamu ya pili itafuatia hapo mwezi wa Mei, na wanajeshi waliobakia, watarejeshwa nyumbani mwezi wa Oktoba.
Ukraine hivi sasa ina wanajeshi 1,650 nchini Irak. Kwa kufanya hivi, bwana JUSCHT-CHENKO anatekeleza ahadi aliyotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.