KIEV : Rais wa zamani kuhojiwa kwa mauaji ya mwandishi
6 Machi 2005Matangazo
Rais wa zamani wa Ukraine Leonid Kuchma amerudi Kiev ambapo anategemewa kuhojiwa juu ya mauaji ya mwandishi habari mpinzani.
Kuchma amewasili nchini humo siku moja baada waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani Yury Kravchenko kukutikana amekufa kwa kile kilichoelezwa kuwa amejiuwa.Kifo cha Kravchenko kimekuja ikiwa imebakia masaa machache tu kabla ya kukutana na waendesha mashtaka kujibu masuali juu ya mauaji ya mwandishi habari za uchunguzi Georgy Gongadze ambaye alikuwa akimpinga Kuchma.
Gongadze alitoweka hapo mwezi wa Septemba mwaka 2000 na mwili wake usiokuwa na kichwa ulikuja kupatikana miezi miwili baadae.