KIEV: Msoshalisti achaguliwa spika wa bunge
7 Julai 2006Matangazo
Katika tukio la kushangaza bunge nchini Ukraine limemchagua msoshalisiti Oleksander Moroz kuwa spika wake. Moroz alishinda kura 238 kati ya kura zote 450 akisaidiwa na chama kinachoegemea upande wa Urusi cha rais wa zamani wa Ukraine, Victor Yanukovic.
Hata hivyo vyama vitatu vya muungano wa machungwa vilivyounda serikali vilimpendelea mgombea mwingine na havikushirika katika upigaji kura huo.
Kuchaguliwa kwa Moroz huenda kukasababisha kuundwa kwa muungano mpya na kuyazika matumaini ya Yulia Tymoshenko, mwanaharakati mkubwa katika mapinduzi ya Ukraine mwaka wa 2004, kuchukua tena wadhifa wa waziri mkuu.