KIEV: Kura ya kumuidhinisha Yanukovich kufanyika kesho
3 Agosti 2006Matangazo
Spika wa bunge nchini Ukraine, Oleksandar Moroz, amesema kura ya kumuidhinishaViktor Yanukovich kuwa waziri mkuu mpya wa Ukranine imeahirishwa hadi kesho.
Moroz amesema kucheleweshwa kwa kura hiyo kunahitajika ili kuvipa vyama wakati wa kuunda serikali mpya ya muungano, itayoujumuisha muungano wa rais Viktor Yuschenko.
Uamuzi wa rais Yuschenko kumpendekeza Viktor Yanukovich awe waziri mkuu mpya, ulifuatia mazungumzo ya dharura yaliyonuia kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Ukraine na kumzuia rais Yuschenko kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya.