Kiev. Fischer aiunga mkono serikali ya Ukraine.
22 Machi 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Bwana Joschka Fischer amesema anaunga mkono serikali mpya ya Ukraine inayounga mkono mataifa ya magharibi. Bwana Fischer, ambaye yuko mjini Kiev, amekutana na mawaziri wenzake wa Ukraine na Poland Boris Trasyuk na Adam Rotfeld jana wakijadiliana kuhusu uwezekano wa Ukraine kuingia katika jumiya ya Ulaya hapo baadaye.
Bwana Fischer amesema kuwa anamatumaini kuwa democrasia katika Ukraine italeta ukuaji wa kiuchumi na kuanzisha mahusiano ya wazi na umoja wa Ulaya EU. Ameongeza kuwa Ujerumani na Poland zote zitaiunga mkono Ukraine katika juhudi zake za kutaka kujiunga na shirika la kibiashara la kimataifa , WTO.