KHARTOUM. Wanajeshi wa Ujerumani kuhudumu Sudan.
14 Aprili 2005Matangazo
Serikali ya shirikisho la Ujerumani limepitisha azimio la kuwapeleka wanajeshi wake 75 kujiunga na walinda amani wengine 750 wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan.
Tangu kutiwa saini mkataba wa amani baina ya serikali na Waasi wa Kusini mwa Sudan ambao umesimamisha mapigano ya miaka 21 iliyopita Umoja wa Mataifa ulipitisha pendekezo la kuwapeleka wanajeshi wa kulinda amani 10,000 kufikia mwisho wa mwezi jana.
Uamuzi huo wa baraza la mawaziri wa Ujerumani wa kuwapeleka wanajeshi wa Bundeswehr kujiunga na walinda amani wengine wa umoja wa mataifa huko nchini Sudan sasa unasubiri kupitishwa na bunge la Ujerumani.