KHARTOUM: Sudan na Chad zasaini mkataba
27 Julai 2006Matangazo
Sudan na Chad zimesaini mkataba unaolenga kumaliza hali ya wasiwasi katika eneo la mipaka yao. Nchi hizo zimekubali kumaliza tofauti zao kwa njia ya kidiplomasia.
Kuna mpango wa kupeleka kikosi cha wanajeshi kutoka Chad na Sudan watakaoshirikiana pamoja kulinda usalama katika eneo la mpakani.
Serikali ya Sudan na serikali ya Chad zimekuwa zikilaumiana kwa kuwaunga mkono waasi katika vita vya kikabila vilivyoanza mwaka wa 2003 katika jimbo la Darfur.