SiasaIran
Khamenei: Raia wa Iran tuungane dhidi ya mipango ya Marekani
24 Agosti 2025Matangazo
Khamenei ameyatoa matamshi hayo siku ya Jumapili katika msikiti mmoja mjini Tehran, akisisitiza kuwa baada ya mashambulizi ya Marekani na Israel, maafisa wa Marekani walikutana barani Ulaya ili kujadili serikali inayopaswa kuitawala Iran baada ya kuuangusha utawala uliyopo.
Kiongozi huyo mkuu wa Iran ambaye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu masuala ya serikali, amesema nchi yake imejizatiti na imeungana na kwamba ilivishinda vita vya siku 12 mwezi Juni dhidi ya Israel, lakini akatahadharisha kuhusu migawanyiko ya ndani aliyosema inachochewa na mataifa ya kigeni.