MigogoroIran
Khamenei asema vitisho vya Trump kwa Iran havitofika popote
21 Machi 2025Matangazo
Khamenei ameyasema hayo kupitia hotuba iliyorushwa moja kwa moja na televisheni katika kile kinachozingatiwa kuwa jibu kwa matamshi yaliyotolewa na Rais Donald Trump hivi karibuni aliyesema Marekani inaweza kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran.
Soma pia: Iran, China na Urusi kuanza luteka za pamoja za kijeshi
Kwenye hotuba yake Khamenei pia amekanusha madai kwamba nchi yake inafadhili vita vya kiwakala kwenye kanda ya Mashariki ya Kati akisema makundi yanayotajwa yanafanya kazi kwa uhuru bila mkono wa Tehran.
Rais Trump aliitaka Iran ikomeshe uungaji mkono wa kijeshi kwa makundi ya wapiganaji kwenye kanda hiyo ikiwemo Hamas na Waasi wa Houthi wa nchini Yemen ama ijiandae "kulipa matokeo ya ufadhili wake"