Khamenei akutana na viongozi waandamizi wa Hamas huko Tehran
8 Februari 2025Viongozi hao waliokutana na Khamenei ni Kaimu kiongozi wa Hamas Khalil al-Hayya na viongozi wengine wawili wa kundi hilo ambao ni Mohammad Darwish, mkuu wa baraza la uongozi la Hamas, na afisa mkuu Nizar Awadallah.
Khamenei ambaye taifa lake linawaunga mkono Hamas kwenye vita vyao na Israel , amewaambia wajumbe hao kuwa wameushinda utawala wa Kizayuni na ambao kwa hakika ni pigo pia kwa Marekani kwa akisema kundi hilo halikuwaruhusu kufikia malengo yao.
Televisheni ya Iran imesema viongozi hao wa Hamas walikuwa ziarani mjini Tehran ili kumpongeza Khamenei kufuatia kumbukumbu ya mapinduzi ya serikali ya Kiislamu ya mwaka 1979 na kushukuru pia hatua ya uungwaji mkono na msaada usioyumba wa Iran.
Hayo yanajiri wakati leo hii, Hamas imewaachilia mateka watatu wa Israel kwa kubadilishana na wafungwa 183 wa Kipalestina, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya usitishwaji mapigano huko Gaza.