Kesi ya Diego Maradona hatarini baada ya jaji kujiondoa
28 Mei 2025Julieta Makintach alijiondoa kwenye kesi hiyo baada ya kufichuliwa kuwa amekuwa akishiriki katika filamu inayotengenezwa kuhusu kesi hiyo maarufu katika ulimwengu wa kandanda. Maradona alifariki Novemba 2020 akiwa na umri wa miaka 60, baada ya kufanyiwa upasuaji wa ubongo.
Jopo lake la madaktari saba wanakabiliwa na kesi kuhusu mazingira ya kumuuguza nyumbani kwake, ambayo waendesha mashitaka wanaeleza yalikuwa ni uzembe mkubwa. Baada ya mfululuzo wa misako ya polisi na kufungiwa kwa wiki moja kujihusisha na kesi hiyo, Makintach mwenye umri wa miaka 47 alituhumiwa mahakamani jana kwa kukiuka maadili ya kutoegemea upande mmoja, ushawishi wa biashara na hata rushwa kuhusiana na jukumu lake katika filamu hiyo.
Soma pia: Ulimwengu wa soka wamlilia Diego Maradona
Kuondolewa kwake ni aibu kwa mfumo wa mahakama wa Argentina na kunaweza kukatiza kesi hiyo inayofuatiliwa na mashabiki wa soka duniani kote.