SiasaAsia
Korea Kusini yaanza kuskililiza kesi ya Yoon Suk Yeol
20 Februari 2025Matangazo
Yoon mwenye umri wa miaka 64 anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha uasi na matumizi mabaya ya madaraka, yanayotokana na hatua yake ya kutangaza amri ya kijeshi Desemba 3 mwaka jana nchini humo.
Hatua hiyo ilionekana kama mpango wake wa kujaribu kuwaandama wapinzani wake wa kisiasa, lakini iliitumbukiza Korea Kusini katika mkwamo mkubwa wa kisiasa.
Soma pia:Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani ashtakiwa kwa kuongoza uasi
Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap, limeripoti kwamba, kikao cha mahakama cha leo ni cha awali cha kutafuta ufafanuzi kuhusu mashtaka yanayomkabili kiongozi huyo na kuchukuwa hatua zinazofuata. Ikiwa atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha muda mrefu.