Kenya: Tunaunga mkono juhudi za amani Sudan
20 Februari 2025Ikijibu shutuma za Sudan hapo jana, wizara ya mambo ya nje ya Kenya imesema nchi hiyo inawahifadhi wakimbizi wengi wa Sudan na kwamba ina historia ya kuwezesha kufanyika kwa mazungumzo bila nia mbaya.
Kenya yakabiliwa na shtuma mbali mbali
Macharia Munene, profesa wa mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani, USIU, jijini Nairobi, alisema kuwa Kenya inakabiliwa na hatari ya kutengwa kimataifa kwa sababu ya kasoro za sera yake ya kigeni.
Sudan yaishutumu Kenya kwa kuruhusu mazungumzo ya RSF
Aidha, Profesa mwingine katika Chuko Kikuu cha Kimataifa cha Riara, Kisemei Mutisya amesema kuwa utawala nchini Sudanni halali na kuongeza kuwa chini ya sheria za kimataifa, serikali ya Sudan ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na inatambulika kama serikali iliyo madarakani.
RSF yashambulia na kuuwa zaidi ya watu 200 Sudan
Haydar Abdul Karim, mwanaharakati wa amani wa Sudan ambaye pia ni mwandishi wa habari wa kujitegemea anayeishi nchini Kenya, ameliambia shirika la habari la AP kwamba serikali za kikanda hazipaswi kuegemea upande wowote.
Amezitaka nchi za kikanda kujiepusha kuunga mkono uundaji wa serikali ama miungano, na badala yake kuzingatia kushinikiza pande zinazozozana kukaa chini na kujadiliana.
Umoja wa Mataifa yaelezea wasiwasi kuhusu mzozo wa Sudan
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kulingana na wao, kudumisha umoja wa Sudan, uhuru na uadilifu wa kimaeneo, bado ndio njia sahihi ya utatuzi endelevu wa mzozo huo.
Zaidi ya watu 200 wauawa katika siku tatu za mashambulizi ya Sudan
Akizungumzia kuhusu tangazo lililopangwa na RSF la kuunda serikali sambamba, Dujaric ameongeza kuwa wana wasiwasi mkubwa juu ya kuongezeka zaidi kwa mzozo waSudan, na hatua zozote kama hizo, ambazo zinaweza kuongeza mgawanyiko wa nchi hiyo pamoja na hatari ya kufanya mzozo huo kuwa mbaya zaidi.
Sudan yaishtumu Kenya
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan, iliyotiifu kwa mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan, ilikosoa Kenya kwa kuruhusu tukio hilo na kuongeza kuwa hatua hiyo inaongeza mpasuko wa mataifa ya Kiafrika, inakiuka uhuru wao, na kuingilia mambo yao ya ndani.