Kenya yalaaniwa kwa kuwaruhusu waasi wa RSF nchini humo
19 Februari 2025Wizara ya mambo ya nje ya Sudan, iliyo tiifu kwa mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan, imeikosoa Kenya kwa kuruhusu tukio hilo.
Katika taarifa, wizara hiyo imesema hatua hiyo inakuza mpasuko wa mataifa ya Kiafrika, inakiuka uhuru wao, na kuingilia mambo yao ya ndani.
Rais wa Kenya William Ruto pia alikabiliwa na ukosoaji mkubwa nchini mwake.
Soma pia:Sudan yaishutumu Kenya kwa kuruhusu mazungumzo ya RSF
Mukhisa Kituyi, mwanasiasa na ambaye pia aliwahi kuhudumu kama katibu mkuu wa Shirika la Maendeleo na Biashara la Umoja wa Mataifa, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kila anachokifanya Ruto ni kutupilia mbali tahadhari ya jadi na mtazamo wa heshima kwa diplomasia ya Kenya.
Hata hivyo serikali ya Ruto haikujibu ombi la tamko kuhusu hali hiyo.