Kenya inaendeleza juhudi za kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati - maarufu kama STEM. Shirika la Anga la Kenya (KSA) limeanzisha mpango maalum kwa shule za upili kuchangia katika kampeni hii. Makala ya leo ya Sema Uvume inamulika mada hiyo.